Kuhusu Ukombozi

Shule ya Msingi ya Ukombozi ipo katika mkoa wa Iringa, Tanzania, Afrika ya Mashariki. Inapatikana katika nyanda za juu kusini kwa Tanzania. Shule ina darasa la kwanza mpaka la saba.Mbali na majaribio, kazi za kufanya, na mitihani ya mwisho wa muhula, wanafunzi wa darasa la nne wanafanya mtihani ili kufuzu kuingia darasa la tano. Zaidi ya hapo, wanafunzi wa darasa la saba wanafanya mtihani wa taifa, wanaofaulu wanajiunga na shule za sekondari za serikali.

Ukombozi ni jina la Kiswahili linalomaanisha "Liberation". Wanafunzi wengi wanaojiunga wana wastani wa miaka saba. Wasichana wanavaa mashati meupe na sketi za buluu. Wavulana wanavaa mashati meupe na kaptula za buluu. Wanafunzi wanavaa masweta ya kijani kujikinga na hali ya hewa ya "baridi".

Sikuj hizi, kwa kutumia msaada wa Chuo Kikuu cha Tumaini, shule ya msingi ya Ukombozi inatarajia kuwa kundi la Lengo ni kuwa kundi la kimataifa lenye kutoa elimu bora ya kompyuta kwa wanafunzi kwa njia ya kufundisha, warsha, utafiti na machapisho.