Karibu

Shule ya msingi ya Ukombozi ipo katika mkoa wa Iringa, Tanzania, Afrika Mashariki. Ipo nyanda za juu za kusini kwa Tanzania. Shule ina wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la saba. Mbali na majaribio, shughuli za kufanya, na mitihani ya mwisho wa muhula, wanafunzi wa darasa la nne wanatakiwa kufanyamtihani wa kuingia darasa la tano. Zaidi ya hapo, wanafunzi wa darasa la saba wanafanya mtihani wa Taifa, wanaofaulu wanaenda katika shule za sekondari za serikali.